Maafisa Rasilimali Watu wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini wamepatiwa mafunzo ya usafishaji taarifa 'data' kupitia mfumo wa eMsawazo, mafunzo yenye lengo la kuwa na takwimu sahihi za mahitaji ya watumishi wa Umma kwa ngazi ya sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kikao hicho kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala la Mikoa na Serikali za Mitaa, mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia tarehe 29 Septemba, 2025.
Mafunzo hayo yamewakutanisha Maafisa Rasilimali Watu wa mikoa ya Kanda Kaskazini ikujumuisha mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa