Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha wakishuhudia uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, iliyozinduliwa leo mkoani Arusha kwenye viwanja vya Ngarenaro Jijini Arusha ikiwa ni mara ya pili kwa kampeni hiyo kufika mkoani Arusha ndani ya mwezi Machi. Katika Hotuba yake Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Damas Ndumbaro ameeleza kuwa kampeni hiyo itafika kwenye Wilaya na Kata zote za Mkoa wa Arusha kwa siku kumi za utekelezaji wake, akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuwasilisha changamoto zao za kisheria kwa Wanasheria hao wanaotoa huduma hizo bure chini ya ufadhili wa Rais Samia Suluhu Hassan
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa