Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda amekabidhi rasmi Ofisi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Kenan Laban Kihongosi, hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkoa huo mapema leo Juni 30, 2025.
Akizungumza wakati akimkaribisha Mhe.Kongosi, Ndugu Makonda amempongeza Mhe.Kiongosi kwa kuheshimiwa na kuaminiwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani na kumuhakikishia kuwa anamkabidhi wananchi wa Arusha wenye upendo na msikamano pamoja na mkoa huo ukiwa salama.
Katika hotuba yake ya kuaga, Makonda alianza kwa kumshukuru Mungu, na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kuongoza Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha mwaka mmoja alichohudumu huku akiwashukuru wananchi wa mkoa kwa upendo na ushirikiano mkubwa waliompa kipindi chote alichofanya kazi mkoani hapo.
Aidha, ameweka wazi kwa namna anavyofahamu uchapakazi wa Mhe. Kihongosi hana mashaka naye na kumtaka kuendelea kuwatumikia wananchi wa Arusha, wananchi ambao wanaupendo mkubwa huku akimsisitiza umuhimu wa ushirikiano na mshikamano kati yake na viongozi wa mkoa huo wakiwememo viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa dini, wadau na wananchi wa ngazi zote.
“Nina imani kuwa Mkuu mpya wa Mkoa, Mhe. Kenan Kihongosi, ataendeleza jitihada zote tulizoanza na kuongeza ubunifu mpya katika kuleta maendeleo ya wananchi wa Arusha, nikuhakikishie wananchi wa Arusha wote ni wajanja na wapenda maendeleo" amesema Makonda
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa