Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Novemba 29-30 anatarajiwa kuongoza Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC kwenye maadhimisho ya miaka 25 jumuiya hiyo yenye nchi nane wanachama.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumanne ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Viongozi wa dini Mkoani Arusha, akisema uwepo wa Marais hao nane wa Jumuiya ya EAC ni muendelezo wa mikutano mingi ya Kimataifa na Kitaifa inayofungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha na mikoa jirani.
Rais Samia pia kando ya Mkutano huo anatarajiwa kukutana na Viongozi wa jamii ya Kimasai kutoka Wilayani Ngorongoro mkoani hapa ili kujadiliana na kuzungumza nao katika kutafuta maridhiano dhidi ya mgogoro uliopo baina yao kutokana na zoezi linalofanywa na serikali la kuwaondoa ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa