Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda Paul Makonda ameandaa Matembezi ya pamoja na Maombi Maalum ya kuombea Mkoa wa Arusha na Taifa la Tanzania siku ya Tarehe 09 Desemba, 2024.
Matembezi yataanzia Mzunguko wa Impala (Round abou ya Impala) kuelekea Mzunguko wa Clock Tower (round about ya Clock Tiwer) kupitia barabara ya Uhuru (Uhuru Road) na kupandia Mtaa wa Uswahilini (barabara ya St.Thomas Hospital) na kuishia mzunguko wa Mnara wa Mwenge (Makumbusho ya Azimio la Arusha)
Wote mnakaribishwa, Njoo tuzungumze na Mungu juu ya Mkoa wetu wa Arusha, njoo tuseme na Mungu tukiwa tumebeba pamoja bendera ya Nchi yetu ya Tanzania
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa