Mapema leo katika Kongamano la Kuadhimisha Miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika lenye jukumu la kuzuia, kudhibiti na kutatua migogoro katika bara letu. Wakati chombo hiki kinaanzishwa, kilipewa dhima ya kiutendaji katika kushughulikia migogoro na kuimarisha uwezo wa kuleta amani, usalama na utulivu kote barani Afrika, pamoja na kuanzisha majadiliano ya upatanishi hadi kusaidia nchi kujengwa upya baada ya vita, eneo ambalo tumepiga hatua kubwa katika utekelezaji wake.
Katika kongamano hili, nimewatunuku nishani baadhi ya viongozi ambao kwa miaka 20 ya baraza hili wametoa mchango mkubwa katika utendaji wake na kusaidia kukuza amani na ustawi kwenye bara letu, wakiepusha vita na utengano wa jamii mbalimbali.
Mbali na mafanikio tuliyopata, bado tuna kazi ya kujifunza kutokana na historia tuliyopitia ya migogoro mbalimbali katika kipindi hiki cha miaka 20 na kujipanga kwa miongo ijayo, ikiwa ni pamoja na kutambua mabadiliko ya aina ya migogoro na aina ya vitisho vinavyolikabili bara letu kwa sasa.
Mungu Ibariki Afrika.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa