Milioni 469 zimetumika katika ujenzi wa kituo cha afya Mto wa Mbu wilayani Monduli.
Akisoma taarifa ya mradi huo Mganga mkuu wa kituo cha afya Dr. Emma Agostino Msofe, amesema ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka 2017 baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 400.
Pia fedha nyingine zimetoka halmashuri kiasi cha shilingi milioni 30 na wananchi wamechangia milioni 39.
Ujenzi wa kituo hicho cha afya unaendelea na mpaka sasa majengo yaliyojengwa ni jengo la upasuaji, jengo la wazazi,jingo kufulia,nyumba ya utumishi,vyoo vya nje na matenki ya kuhifadhia maji.
Amesema kituo hicho cha afya kitawasaidia wananchi kupata huduma bora za afya na katika mazingira bora.
Nae kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndugu. Charles Francis Kabeho, amesema wananchi wanatakiwa kukitunza kutuo hicho kwa umakini na pia amewataka watumishi watoe huduma bora na kwa weridi kwa wananchi.
Mwengi wa Uhuru ulianza mbio zake mkoani Arusha Mnamo Septamba 12 katika wilaya ya Ngorongoro kisha wilaya ya Karatu na sasa unaendelea katika wilaya ya Monduli.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa