Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchiesimu Mramba, ameelezwa kuwa, Mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati 2024, unaofanyika kwenye ukumbi wa jengo la PAPU Mkoani kuhaki ni fursa kwa nchi yetu ya Tanzania katika kuhakikisha kunakuwa na matumizi bora ya nishati ambayo yatapelekea kupunguza upotevu wa nishati, kupunguza gharama za matumizi ya nishati, kupunguza hewa ukaa pamoja na kutunza mazingira.
Mhandisi Mramba, amesema hayo wakati akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko @biteko kufungua Mkutano wa mapema leo Desemba 04, 2024.
Katibu huyo ameeleza lengo la Mkutano huo ni kujenga uelewa wa pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya matumizi bora ya Nishati baina ya wadau kutoka Ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki na zile Nchi za Kusini mwa AfAfri (SADC).
Aidha, amebainisha kuwa katika mkutano huo, washiriki watapata wasaa wa kujadili changamoto na fursa mbalimbali za masuala ya matumizi bora ya Nishati pamoja na fursa za matumizi bora ya Nishati kikanda
"Mkutano huu umelenga pia kutafuta njia bora ya nchi wanachama wa Jumuiya zote mbili kushirikiana kwenye uandaaji wa viwango na miongozo ya pamoja ya matumizi bora ya nishati, jambo ni fursa kwa nchi yetu ya Tanzania kutokana na umuhimu wake". Amefafanua Mhandisi Mramba.
Awali Kauli Mbiu ya Mkutano ni “Kuchagiza Matumizi Bora ya Nishati kwa Maendeleo Endelevu”.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa