Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya kata halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, wamekula Kiapo muda mfupi kabla ya kuanza mafunzo ya vitendo ya kutumia mashine za mfumo wa kuandikishia wapiga kura (Voters Registration System) kwenye Daftari la kudumu la Wapiga kura, mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Ngorongoro, Desemba 04, 2024.
Mafunzo hayo yametolewa kwa watalamu hao ikiwa ni maandalizi ya Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, linalotarajiwa kufanyika Mkoani Arusha kuanzia tarehe 11- 17 Desemba, 2024.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa