Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha, Mhe.Kenan Laban Kihongosi, amekabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda na kuanza kazi rasmi na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama na Serikali, watumishi wa Umma, viongozi wa dini na mila, pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo, mapema leo mapema leo Juni 30, 2025.
Hafla hiyo ilianza kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu na shughuli za utekelezaji wa mkoa huo huku akieleza mafanikio yaliyopatikana kisekta kwa kipindi chote alichohudumu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu mpya wa Mkoa Mhe. Kihongosi, amemshukuru Mwenyenzi Mungu kupitia Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan kwa imani yake kubwa na kumpa dhamana ya kuongoza Mkoa wa Arusha na kumshukuru Mtangulizi wake Ndugu Makonda kwa kazi kubwa aliyoifanya katika mkoa huo, kazi ambayo ameacha alama kubwa mkoani hapo.
"Mhe.Rais amenituma Arusha kuja kuwatumikia wananchi wa Arusha na nimekuja kufanya kazi, ninachoomba kwenu ni ushirikiano ili kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo, tukiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wa Arusha wanafurahia matunda ya nchi yao". Ameweka wazi Mhe.Kihongosi
Aidha, amesisitiza kutoruhusu kikwazo chochote kitakachozuia agenda ya maendeleo katika utendaji kazi, wajibu wake ni kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiweo matumizi sahihi ya fedha za Umma zinazoletwa kwa ajaili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Tutakutana site, tutafanya ziara wilaya zote, tutakagua miradi ya maendeleo, tutasikiliza na kutatua kero za wananchi, Hatutamuacha mtu nyuma, kwa kuzingatia huu ni mwaka wa uchaguzi, Viongozi bora wakatambulike kwa zilizofanywa na serikali". Amesema
Zaidi amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kwa kusimamia Kanuni, Sheria na taratibu kwa kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wote, ili kila mtua aweze kufurahia matunda ya Serikali na Nchi yake.
Awali Mhe.Kihongosi amehamishiwa mkoani Arusha akitokea Mkoa wa Simiyu kufuatia mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na Mhe. Rais na kuagizwa kuja kuwaaunganisha wanaArusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa