Wasomi wametakiwa kutumia elimu yao kutatua changamoto zilizopo katika jamii zao, ili waweze kujipatia vipato na pia kusaidia jamii hizo.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta alipokuwa akizindua rasmi upango wa kuwaendeleza kwa ujuzi wanafunzi wa masomo ya Sayansi kutoka katika shule mbalimbali za Mkoa wa Arusha ujulikanao kama (Future stem for Business Leaders).
“Nimefurahishwa sana na mpango huu ambao unawapa nafasi wanafunzi wa shule za sekondari kujifunza zaidi ya darasani.
Mpango huu umeanzishwa na wataalamu mbalimbali kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam na Chuo cha Nelson Mandela chini ya kampuni ya Gongali Model.
Amewataka vijana hao kuchangamkia fursa hiyo ya kutumia elimu kwa kujiajiri na kuajiri wengine ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi.
Amesema mpango huo utawasaidia vijana kuacha kutegemea kuajiriwa tu bali wataweza kujijenga katika kujiajiri.
Dkt. Innocent Lugendo Muhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam pia ni mmoja wa waanzilisha wa mpango huo, amesema lengo kubwa la mradi huo ni kuwawezesha wanafunzi hasa wa masomo ya sayansi kutumia elimu yao kutatua changamoto katika jamii zao kwa kuzalisha ajira na biashara.
Amesema mradi huo utawasaidia vijana kuweza kujisimamia katika uchumi na kuendesha maisha yao ya kila siku.
Mradi wa Future stem business for Leaders ulianza 2017 Dar es Salaam na sasa umezinduliwa rasmi Jijini Arusha na utakuwa ukifanyika katika sule 15 za sekondari za Jijini Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa