Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewahimiza wakazi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la Mkazi ili kuweza kupata sifa za kushikiri kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadae Novemba 27 ya mwaka huu.
Mara baada ya kukagua zoezi la uandikishaji kwenye vituo mbalimbali Jijini Arusha, akiwa kwenye Kituo cha kujiandikishia wananchi kilichopo kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata ya Moivo Jijini Arusha, Mhe. Makonda amewaambia wananchi kuwa maendeleo ya Taifa lolote lile yanaanzia ngazi ya Kitongoji na Kijiji na hivyo kuwataka kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi huo ili kuwapata viongozi waadilifu na wenye kutanguliza mbele maslahi ya umma.
Uchaguzi wa serikali za Mitaa unafanyima Novemba 27, 2024 na kwasasa kulingana na ratiba ya uchaguzi huo, kwasasa zimesalia siku tano pekee kwa wananchi wenye sifa kuweza kujiandikisha kwenye daftari la Mkazi ili kuruhusu wananchi kuweza kuchagua na kuchaguliwa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa