Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella amemkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Charles Rashid Mkombachepa, Lori la Kliniki Tembezi (mobile clinic) na kuagiza kuanza, mara moja, kufanya kazi kwenye halmashauri ya Ngorongoro.
Mhe. Mongella ameweka wazi kuwa, Lori hilo la Kilini tembezi, limeletwa kufuatia mkakati wa uboreshaji na uimarishaji wa huduma za Afya, hususani huduma za dharura na kuongeza kuwa, mkoa unaanza rasmi utekelezaji huo, kwa kuelekeza Lori hilo kutumiwa na Madaktari Bingwa, kutoa huduma kwa wagonjwa walio kwenye maeneo ya pembezoni, ambayo hayafikiki kwa wepesi.
Mhe. Mongella, hakusita kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwajali wananchi wa Arusha, ambao Jiografia ya maeneo mengi ni magumu na hayafikiki kwa wepesi na watu wake wanaishi kwa mtawanyiko mkubwa, ambao wanahitaji huduma za afya kuwafikia kwa karibu.
Aidha, Mhe. Mongella amemsisitiza Mganga Mkuu wa mkoa, kuhakikisha anawapangia Madaktari Bingwa, kwenye halmashauri za pembezoni kwa kuanza na wilaya ya Ngorongoro, Longido na baadhi ya maeneo ya Arumeru, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ndani ya maeneo yao, kama yalivyo malengo ya Serikali.
"Mama Samia ameshafanya kazi yake, kaai iliyopaki ni sisi kumsaidia kuhakikisha wananchi wanapata huduma, ninakuagiza Mganga Mkuu, gari hili likafanye kazi iliyokusudiwa ya kuwahudumia wagonjwa kwenye maeneo yao, madaktari wapangiwe na kuanza kazi kwenye wilaya ya Ngorongoro na madaktari walifuate gari hilo na kutoa huduma kwa wananchi, kwenye maeneo yao" Amesisistiza
Awali, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Mkombachepa, amesema kuwa, wamepokea magari manne yenye thamani ya shilingi milioni 646.3, kutoka Serikali kupitia Ofisi ya Rais - TAMISEMI, ikiwa ni mkakati wa Serikali wa uboreshaji na uimarishaji wa huduma za afya hususani huduma za dharura na rufaa pamoja na kusogeza huduma zaidi karibu na wananchi.
Amefafanua kuwa, magari hayo manne aina ya Toyota Land Cruiser Ambulance 3, zimegawiwa kwenye wilaya ya Ngorongoro, Longido na Hospitali ya Rufaa mkoa wa Arusha, huku Lori la Kliniki Tembezi likikabidhiwa Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa kwa ajli ya kufanya kazi za kutoa huduma kuzunguka mkoa mzima.
Hata hivyo, Dkt. Mkombapepa kwa niaba ya watumishi wa Afya, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita, kwa kuwa na mkakati wa kutoa vitendea kazi kwenye Idara ya afya, vieteneakazi ambavyo vinakwenda kuwarahisishia kazi wahudumu hao, huku akiahidia kusimamia utunzania na matumizi sahihi ya vifaa pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki.
#ArushaFursaLukuki
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa