• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA AAGIZA UONGOZI WA LONGIDO DC KUJENGA MOCHUARI KITUO CHA AFYA KETUMBEINE

Posted on: February 2nd, 2024


Na Elinipa Lupembe 


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, ameuagiza uongozi wa wilaya ya Longido kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, kuchukua hatua za haraka kujenga chumba cha kuhifadhia maiti (mochuari) kwenye kituo cha Afya Ketumbeine, kituo ambacho kimejengwa na fedha kutoka Serikali kuu, zaidi ya shilingi milioni 500.


Mhe. Mongella ametoa agizo hilo mara baada ya wananchi wa Ketumbeine, kulalamikia uwepo wa changamoto hiyo, unaowalazimu kutumia gharama kubwa kwenda kuwahifahi wapendwa wao, Longido mjini umbali wa Km 90 mpaka 120, wakati wa mkutano wa Hadhara, uliowakutanisha wakazi wa Tarafa ya Ketumbeine, kwenye kijiji cha Lopolosek.


"DC na Mkurugenzi, tusisubiri kila kitu kufanyiwa na Serikali Kuu, wametoa fedha za kukamilisha Kituo cha Afya, tumieni mapato ya ndani kujenga chumba cha  mochuari, sio lazima kusubiri kila kitu kusubiri kufanyiwa na Serikali Kuu, jiongezeni, ninawapa mwezi mmoja, nitakuja kugungua mochuari hiyo"  Mhe Mongella


Awali, akiwasilisha Kero hiyo, Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Longido Joseph Laizer, ameishukuru Serikali na kuipongeza kwa miradi mingi inayoteklezwa kwenye Tarafa hiyo ya Ketumbeine, husasni ujenzi wa Kituo cha Afya, kituo ambacho amaekiri ni cha kisasa na kinatoa huduma nzuri  kwa wananchi hao.


Aidha, ameeleza changamoto kubwa ya afya inayowakabili wanachi hao, ni ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti, na kumuomba mkuu huyo wa mkoa kuona namna ya kujenga chumba hicho kwenye kituo chao cha Afya.


"Mhe. Mkuu wa mkoa, wanachi wa Ketumbeine, tunatambua na kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani, ombi letu kubwa, ni kupata chumba cha mochuari kwenye kituo cha afya Ketumbeine, tunatumia gharama kuwa pindi watu wanapofariki kwenda mbali kuhifadhi miili, tunaomba tupate msaada huo, ili huduma hii ipatikane kwenye hospitali yetu" Ametoa ombi hilo mwenyekiti huyo mstaafu.


Awali mkuu wa mkoa wa Arusha, amepokea kero za wananchi hao na kuziagiza Mamlaka husika kuzitatua ndani ya kipindi cha mwezi mmoja mpaka mitatu.

#ArushaFursaLukuki✍




Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa