Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella akikagua mradi wa Ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya wilaya ya Karatu mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 3.5.
Mhe. Mongella ameuelezea mradi huo kuwa ni muhimu kwa wananchi wa Karatu kwa kuwa hakukuwa na hospitali ya wilaya inayotoa huduma zote kabla ya kwenda hospitali ya Rufaa.
Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi kuongeza kasi ya usimamizi na utekelzaji katika hatua za umaliziaji ikiwemo kuweka umeme wenye uwezo wa kuendesha mashine kubwa ikiwemo mashine za kuzalisha Oksijeni, na vifaa tiba ambavyo tayari serikali imekwisha kuvito ili mradi huo ukamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
"Licha ya Mradi kuwa katika hatua za mwishoni DC na Mkurugenzi ongezeni kasi ya kukamilisha mambo ambayo ni ya muhimu, fuatilieni TANESCO ili kufikisha umeme wenye nguvu ya kusukuma mitambo hii, ifikapo Novemba 30 mradi uwe umekamilika na kutoa huduma zote"
Zaidi amewataka watoa huduma kuhakikisha wanatoa huduma bora ili wanachi waweze kuvutiwa kutumia Hospitali za serikali na sio kwenda kutumia gharama kubwa katika hospitali za binafsi.
Mhe. Rais anasisitiza suala la huduma bora kwa wateja, customer care ndio msingi wa hospitali, Watalamu mliopa kwenye hospitali zetu, Serikali imewaamini na kuwapa dhamana kubwa na muhimu kwa maisha ya binadamu, fanyeni kazi kwa bidii na weledi huku mkitambua mnayo dhamana ya maisha ya watu na sio serikali peke yake" Amebainisha RC
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Juma Hokororo amesekiri kupokea maagizo ya Mheshimiwa mkuu wa Mkoa na kuahidi kuongeza kasi ya usimamizi wa mradi huo, na kufafanua kuwa tayari wamekwisha kufanya mawasiliano na TANESCO na mchakato wa kubadilisha Transfomer umefanyika na anaamini umeme utafika hospitalini hapo na vifaa vyote kuanza kutumika.
"Kipekee tunamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujenga Hospitali ya wilaya, ni hitaji la wananchi na tayari licha ya kwamba bado tunaendela na ukamilishaji lakini tayari huduma za nje zimeanza kutolewa"Ameema Hokororo
Awali Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo amesema kuwa kwa sasa hospitali imeanza kutoa huduma na kuhudumia wagonjwa thelathini kwa siku
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa