• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA: AWAMU YA SITA YATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO YA TAKRIBANI TRILIONI MBILI KISEKTA

Posted on: December 13th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Serikali ya awamu ya sita, kuelekea miaka mitatu ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoa wa Arusha umekuwa miongoni mwa mikoa nchini, iliyonufaika sana kwa kupata miradi mingi ya maendeleo, inayokwenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.


Akizungumza wakati akitoa salamu za mkoa wa Arusha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Hamad Mchengerwa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita imetofa takribani trilioni 2 za kutekeleza miradi ya maendeleo, miradi ambayo imeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii ikilinganishwa na awamu zilizotangulia.


Amesema kuwa, kiasi hicho cha fedha kinaweza kulinganishwa na fedha za miradi kwa miaka sita na kuongeza kuwa  ipo miradi mikubwa ambayo haijawahi kutekelezwa katika mkoa huo, ikiwemo ujenzi wa shule mpya za sekondari na msingi, ujenzi wa vituo vipya vya afya na hospitali mpya za wilaya na mkoa, miradi ambayo inameshaanza kuleta matokeo makubwa sana kwa wananchi wa Arusha.


 "Kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Arusha, tunaipongeza Serikali, kwa namna imeweza kuteleza Ilani ya CCM ya 2020 - 2025, tunampongeza na kuahidi kumuunga mkono,  Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wa Arusha, tunaahidi  kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo za mkoa wetu"


Amesisitiza kuwa, kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo, mkoa unakwenda kupokea magari 9 leo, kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za afya, jambo ambalo halijawahi kutokea zaidi  linajidhihirisha wazi, Serikali ya mama Samia imedhamiria kuondoa kero za wananchi, kuwahudumia wagonjwa katika maeneo yao pamoja na kuondoa vifo vya mama na mtoto.


Hata hivyo,Mhe. Mchengerwa amewapongeza viongozi wa mkoa wa Arusha, kwa kazi nzuri ya usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo, inayotekelezwa katika mkoa huo, pamoja na ushirikiano mkubwa wa viongozi wa Chama na Serikali, ushirkiano  unaosababisha hali ya amani na utulivu kwa wananchi wa mkoa huo.


"Ninawapongeza viongozi wote wa mkoa wa Arusha na Manyara, kwa ushirikiano wa karibu baina ya viongozi wa Chama na Serikali ni chachu ya mafanikio ya Serikali na wananchi, kila kiongozi wa aliyeteuliwa na kuchaguliwa anao wajibu wa kutekelza majukumu yake huku akitambua wote wanajenga nyumba moja" Amesema Mhe. Mchengerwa


Awali, Mhe. Mchengerwa,  amekabidhi magari 13 yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya Usimamizi Shirikishi wa Shughuli za Afya kwenye mikoa ya Arusha na Manyara, huku Arusha ikipata magari 5 na Manyara magari 8, shughuli iliyofanyika leo tarehe 13.12.2023 kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa