• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA MADEREVA KATIKA UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA

Posted on: August 20th, 2024

Na Elinipa Lupembe 


Serikali ya awamu ya sita imekiri kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na madereva wa Serikali katika kukuza uchumi wa Taifa la Tanzania kwa kuzingatia majukumu yao na umuhimu wake.


Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa, wakati akifungua Kongamano la tatu la Madereva wa Serikali, linalofanyika mkoani Arusha kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha, Agosti 20,2024.


Kada hii ya udereva ni muhimu kwa Serikali kutokana na huduma wanayoitoa kwa viongozi na Maafisa wa Serikali, kada ambayo injini inayochochea maendeleo ya Taifa la Tanzania ikiwa inagusa jamii moja kwa moja na kuwasisitiza kufanya kazi kwa weledi.


"Madereva wa Serikali fanyeni kazi kwa uadilifu, simamieni maadili ya kazi kwa kuzingatia mahusiano mazuri mahala pa kazi, nidhamu kazini ni suala la msingi sana, kuheshimu alama za barabarani kwa kuzingatia usalama wa barabarani unaanza na wewe, lindeni usalama wa abiria na waenda kwa miguu pamoja na usalama wa vifaa vinavyotumika"Amesema Waziri Mkuu


Hata hivyo, Waziri Mkuu, ameweka wazi kuwa, Serikali itaendelea kuboresha miundo ya kiutumishi kwa madereva ili kuboresha maslahi yao, huku ikiwa imefanya mapitio ya miundo hiyo na kufanikiwa kubadilisha miundo ya madereva 1, 600 pamoja na kutoa vibali vya ajira mpya, jambo ambalo limechangia idadi ya madereva kuongezeka.


Ameongeza kuwa, Kongomano hilo likatoe hamasa ya madereva kwenda kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia taratibu maadili ya udereva, kanuni, taratibu za utumishi wa Umma pamoja na miongozo ya Serikali, hali itakayoipa heshima kada ya udereva kuwa kama kada nyingine.


Tunafahamu malengo ya chama ni kuikuza kitaaluma na kada ya udereva, kukemea matendo maovu yanasababisha kuiondolea heshima kazi ya serikali, kuongeza umakini na uzingatiaji wa usalama barabarani unakuwa ni kipaumbele cha kila dereva.


"Niwapongeze kwa kuwa Chama hiki kinaendelea kukua na kuwa na sauti kubwa ndani ya Serikali, viongozi wa chama na wizara simamieni madereva kukutana kila mwaka ili kujadili mafanikio na changamoto zao, kukutana kwao kunatoa fursa ya kuboresha utendaji kazi kwa kubadilishana uzoefu, kujadili mambo muhimu  kada hii na kuziwasilisha Serikalini ili zifanyiwe kazi" Amesema Mhe. Majaliwa


Hata hivyo Waziri Mkuu, amefurahishwa na kauli mbiu ya Dereva Jitambue, Timiza Wajibu wako, Usalama Barabarani Unaanza na wewe" ambayo imebeba ujumbe muhimu na wa kipekee hasa kwa  madereva na maslahi ya taifa, kwa kutambua na ufahamu majukumu yao, dhamana ya kuwahudumia viongozi na wananchi na umuhimu wa kutekeleza majukumu na kuzingatia sheria na usalama wa barabarani.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa