• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI KUPITIA BENKI YA TADB KUMUWEZESHA MFUGAJI ARUSHA KUPATA ENEO LA MALISHO.

Posted on: January 10th, 2024

Na Elinipa Lupembe.


Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB, imejipanga kumuwezesha mfugaji wa ng'ombe wa maziwa Bi. Teddy James, wa kata ya Sombetini Jiji la Arusha, kwa kumpatia fedha kwa ajili ya kununu eneo kubwa la malisho pamoja na kumjengea uwezo wa kukuza mtaji wa biashara hiyo ya ufugaji.


Akizungumza mara baada ya kumtembelea mfugaji huyo na kujionea hali halisi ya ufugaji bora anaoufanya, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, licha ya kuridhishwa na kufurahishwa na kazi kubwa anayoifanya mfugaji huyo, amekiri kumuunga mkono, kwa kusimamia upatikanaji wa eneo kubwa kwa ajili ya malisho  pamoja na upatikanaji wa fedha kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB.


Mhe. Mongella amemsifia na kumpongeza mfugaji huyo,  kwa mradi mzuri wa ufugaji wa kisasa anaoufanya katika eneo dogo la mjini, huku akiahidi kuendelea kumsimamia

na kuhakikisha, anapata eneo kubwa kwa ajili ya kupanua shughuli hizo za ufugaji sambamba na kuhakikisha benki ya TADB inampatia fedha kwa ajili kununua eneo na kukuza mtaji wa biashara yake.


"Inafurahisha sana kwa mtanzania kama Teddy, anafanya biashara kubwa kama hii ya ufugaji wa kisasa, biashara ambayo kama Serikali tutamuunga mkono, ili aifanya kwa ukubwa zaidi na kupanua soko la ndani na nje ya nchi, licha Teddy kufanya ufugaji wa kisasa lakini anafanya biashara ya kuuza maziwa zaidi ya lita 1000 kwa siku  kuuza mitamba na ng'ombe wakubwa kwa wafugaji wengine, kama Serikali ya Mkoa, ninaahidi kusimamia ukuzaji wa mtaji wake" Amesisitiza Mhe. Mongella


Aidha, ameweka wazi kuwa, asili ya wenyeji wa Mkoa wa Arusha ni wafugaji, wanohitaji kuendana na mabadiliko ya maendeleo ya dunia, kwa kufanya ufugaji wa kisasa  kama ilivyo kwa Teddy, Serikali inahitaji watanzania wajasiriamali wa mifugo wengi zaidi.


Hata hivyo, Mhe. Mongella ameweka wazi kuwa, tayari benki ya Kilimo, iko kwenye hatua za mwisho za kumpa mkopo, ili kukuza mtaji na kuongeza uzalishaji, huku  Mkoa ukiendelea kumpa ushirikiano na utalaam ili  mfugaji huyo aendelee kukua zaidi.


Naye Bi Teddy James,  ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kuwawezesha watanzania hususani wafugaji kwa kuwa na programu za kutoa fedha nyingi ili kuwainua, amesema kuwa, tayari Benki ya TADB, imeridhia kumpa fedha ili aweze kununua eneo pamoja na kukuza mtaji na kuongeza uzalishaji kwenye biashara yake ya ufugaji.


"Ninaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa mama Samia, binafsi ninamuunga mkono kupita kauli yake  ya Kazi Iendelee, ninafuga ng'ombe zaidi ya 120 na kupata maziwa lita 1000 kwa siku, ambayo ninahudumia kiwanda cha maziwa cha  Kilimanjari Fresh, ninauza mitamba na ng'ombe wakubwa kwa wafugaji wanaohitaji ng'ombe bora wa maziwa" Amesema Teddy


Awali, mtoto wa mfugaji huyo, mwenye shahada ya Biashara na Uhasibu, CPA. Mariamu, amesema ameamua kuachana na swala kufuta ajira serikalini,  na kujikita kwenye ufugaji huku akiwasisitiza vijana wengi kujiajiri na sio kutegemea ajira kutoka serikalini pekee.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa