Na Prisca Libaga.
Serikali kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2017 hadi 2023 imefanikiwa kuvunja mtandao wa usafirishaji haramu wa dawa za kulevya 'ketamine' zenye uzito wa kilo 405, kutoka nchi za Ulaya kuja nchini Tanzania kwakutumia vibali vya kughushi.
Hayo yameelezwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kukevya (DCEA) Aretas Lyimo katika halfa ya utiaji saini hati ya ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye athari za kulevya, iliyofanyika mkoani Arusha.
Jenerali Lyimo amesema kuwa kundi la vijana wasomi wa vyuo vikuu ndio linaloongoza kwa matumizi makubwa ya dawa za kulevya ikiwemo uchepushwaji wa kemilaki vashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.
Amefafanua kuwa ukamataji zaidi ulihusisha dawa za pethidine chips (ampoules) 7,026, fentanyl (ampoules) Chula 4,260 na Morphine Chula 250 zilizoingizwa nchini kutokea nchi jirani kupitia mipakani,huku kemilaki bashirifu zaidi ya tani601 na zaidi ya Lita 85 zilizuiwa kuingia nchini kutokana na ukiukwaji wa sheria za udhibiti.
#ArushaFursaLukuki
#KaziInaendelea
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa