• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YAPONGEZWA KUTENGA BILIONI 8 ZA KUPANGA ENEO LA UWANJA WA AFCON..

Posted on: November 10th, 2024

SERIKALI YAPONGEZWA KUTENGA BILIONI 8 ZA KUPANGA ENEO LA UWANJA WA AFCON

Serikali  kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepongezwa kwa kutenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 8 kwaajili ya kuanza kutekeleza mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) katika eneo lililopo pembezoni unapojengwa Uwanja wa mpira wa Afcon kata ya Olmoti Jiji la Arusha, mkoani Arusha.

Pongezi hizo zimetolewa na wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea eneo hilo, kujionea eneo unapotekelezwa mradi huo wa KKK pamoja na kujionea maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Afcon,  unaojengwa kwaajili ya mashindano ya mpira Afrika mwaka 2027.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati  Mhe. Najma Murtaza Giga, amesema kuwa, tukio hilo ni la kihistoria ambapo Serikali imejipanga kukamilisha mradi wa ujenzi ndani ya miaka miwili na kuwataka wakandarasi kuongeze kasi ya upimaji wa maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kuanisha makazi na shughuli mbalimbalimbali za maendeleo zitakazofanyika kwenye eneo hilo.

"Arusha ina historia yake kwa utalii na fursa zingine hivyo tunahitaji taarifa kamili juu ya mradi huu ili tuweze kuishauri Serikali katika kuhakikisha vipaumbele vya awali vinapatikana na fursa za uwekezaji zinakuwepo kwani Afcon haipo mbali lazima tujipange". Amesema.

Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema fedha hizo zimetolewa na wizara hiyo kwaajili ya ulipaji wa ekari 207 za awali kati ya ekari zaidi ya 4,575.5 zilizopo katika mpango wote ambapo uwanja wa Afcon pekee una ekeri 83.

"Wizara imetenga fedha hizi kwa ajili ya kuanza ulipaji fidia na tunategemea tukimaliza kupima viwanja hivi tutanunua vingine hapo badae kadri wizara itakavyopata fedha kwaaajili ya kupima, kupanga na Kumilikisha lengo letu mji wa Arusha na maeneo mengine nchi nzima yapangwe". Amesema.

Mjumbe wa Kamati hiyo na mbunge wa Tabora, Mhe. Emmanuel Mwakasaka, amepongeza wizara hiyo kwa kuja na mkakati huo wa upimaji maeneo nchi nzima na kumshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa Uwanja huo wa Afcon.

@wizara_ya_ardhi @bunge.tanzania

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa