ARUMERU:
Na Prisca Libaga Arusha
Shehena ya Bangi ikihusisha magunia 237 na kilo 310 za mbegu imeteketezwa kwa moto kufuatia operesheni iliyofanywa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi Usalama katika Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, operesheni iliyosimamiwa na Mamlaka hiyo Kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Ni katika operesheni ya kupambana na kilimo na biashara haramu ya Bangi kilichoshamiri eneo la Kisimiri wilaya ya Arumeru ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Emmanuela Kaganda amesema lengo ni kubadilisha mtazamo wa wananchi katika kilimo na biashara ya Bangi
Innocent Masangulla ni Mkuu wa Operesheni wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa Mikoa ya Kanda ya kaskazini amesema Operesheni hiyo ni ya tatu kufanyika Arumeru
Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Arumeru wamesema ni vyema serikali ikaongeza nguvu ya Kupambana na kilimo na biashara ya bangi Arumeru.
Mwisho.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa