Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema Tanzania itaendelea kuwa mwenyeji na kuendelea kusapoti Jumuiya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (ECSA) inayowaleta pamoja wataalamu wa Afya kutoka nchi wanachama na dunia Kwa Ujumla.
Dkt. Mpango ameyasema hayo Mkoani Arusha Katika Kilele Cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Jumuiya ya Afya ya nchi wanachama wa ECSA, ambapo nchi zaidi ya tisa zimekutana kusheherekea maadhimisho hayo yaliyo tanguliwa na Mkutano wa siku tatu wa kupata Majibu ya tafiti Mbalimbali Zilizofanywa na wataalam Mbalimbali wa afya duniani.
Akizungumzia faida ya Tanzania Kuwa wenyeji wa Mkutano huo Waziri wa Afya Ummy mwalimu amesema ni pamoja na Jumuiya hiyo kutoa msaada wa kiufundi katika Masuala ya afya nchini.
Naye mgombea aliyependekezwa nchini Tanzania kugombea nafasi ya uwakilishi wa Ukurugenzi wa Shirika la Afya duniani Kanda ya Afrika Dk. Faustine Ndugulile Amesema ni nafasi ya Afrika Sasa nao kushiriki katika kutoa ujuzi wao Elimu ya Afya katika kuboresha Afrika katika Bara zima la Afrika.
Nchi zilizoshiriki katika Mkutano huo ni pamoja na Tanzania, Uganda, Kenya, Zimbabwe, Malawi, Lethoto, Zambia Eswatini, na Botswana ambapo Jumuiya hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 1974 na makao yake makuu yakiwa Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa