• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

TUME YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU YAMPONGEZA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN;  MWENYEKITI WA TUME AMTUMIA SALAMU.......

Posted on: October 28th, 2023

Na Prisca Libaga


Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na Watetezi wa Haki za Binadamu na kutambua mchango wao kwenye maendeleo ya nchi.


Pongezi hizo zimetolewa tarehe 27 Oktoba 2023 na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya Tanzania kuhusu Hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu kwenye kikao cha 77 cha Tume hiyo kinachoendelea jijini Arusha.


Prof. Lumbu amesema kuwa amefurahishwa na taarifa ya Tanzania iliyowasilishwa kwenye kikao hicho kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Serikali na Watetezi wa Haki za Binadamu na kuishukuru nchi hiyo kwa kutambua na kuthamini mchango wa Watetezi wa Haki za Binadamu kama washirika muhimu katika maendeleo ya nchi.


Pia ameeleza kuwa, kauli ya Serikali hiyo ya kufungua milango yake kwa ajili ya kushirikiana na watetezi wa haki za binadamu ni ya kupigiwa mfano na nchi nyingine na kuuunga mkono wito wa Serikali ya Tanzania wa kuwataka watetezi wa haki za binadamu kuendelea kuheshimu katiba ya nchi na miongozo yote inayosimamia haki za binadamu na watu nchini humo.


“Naomba ujumbe wa Tanzania mfikishe salamu zangu za pongezi kwa Mhe. Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na kuwalinda watetezi wa haki za binadamu nchini kwake. Nimefurahishwa pia na kauli ya Serikai ya Tanzania kwamba milango yake ipo wazi wakati wote kwa ajili ya kuwapokea na kushirikiana na watetezi hao wa haki za binadamu,” alisema Mhe. Prof. Lumbu.


Awali akiwasilisha Taarifa ya Tanzania kuhusu Hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Richard Kilanga amesema kuwa Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar zimeendelea kushirikiana na watetezi wa haki za binadamu nchini katika kuboresha masuala yote yanayohusu usimamizi, uimarishaji, na ulinzi wa haki za binadamu nchini.


Amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuyawezesha mashirika hayo na watetezi wa haki za binadamu kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ambapo amesema hadi sasa Tanzania inayo mashirika yasiyo ya kiserikali 9,900.


“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafahamu umuhimu wa watetezi wa haki za binadamu ndiyo sababu zipo sheria mbili zinazosimamia. Ipo Sheria ya Mashirika yasiyo ya kiserikali na Sheria ya Jumuiya za Kiraia kwa pande zote mbili Bara na Visiwani” alisema Kilanga.


Ameongeza kusema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na mashirika hayo katika kukuza na kulinda haki za binadamu na watu nchini pamoja na kujenga uchumi wa nchi ambapo ameeleza kuwa kwa mwaka 2022 mashirika hayo yamechangia kiasi cha Shilingi Trilioni 2.24 sawa na Dola za Marekani milioni 800 kwenye uchumi wa nchi.


“Hakuna shaka kwamba Serikali inatambua mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali, mkiwemo watetezi wa haki za binadamu katika kukuza na kulinda haki za binadamu na watu pamoja na kuleta maendeleo nchini, hususan kwa kuzingatia Mpango Kazi wa Tatu wa Nchi wa Mwaka 2021/22-2025/26 inayotekeleza agenda ya nchi ya Maendeleo ya 2025. Mpango Kazi huu uliandaliwa kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya Kiserikali na kwamba Mashirika hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi huo” alisema Bw. Kilanga.


Kadhalika, Bw. Kilanga amesema kutokana na jitihada za kuimarisha na kusimamia utekelezaji wa haki za binadamu nchini zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, mwezi Mei 2022 ulimtunukia zawadi kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kutetea haki za binadamu na utawala wa sheria nchini.


Vilevile ameongeza kusema milango ya Serikali ipo wazi kwa watetezi wa haki za binadamu katika kuendelea kushirikiana na Serikali ili kutimiza lengo la pamoja la kila mwananchi kunufaika na haki za binadamu na watu huku akisisitiza wajibu wa taasisi za watetezi wa watu wa kuendelea kutii sheria za nchi na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 26 (1).


Kikao cha Kawaida cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kilifunguliwa rasmi jijini Arusha tarehe 20 Oktoba 2023 na kinatarajiwa kumalizika tarehe 09 Novemba, 2023. Pamoja na mambo mengine kikao kinapokea na kujadili agenda mbalimbali zinazohusu haki za binadamu katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.


Mwisho.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa