Vijana wanne wanaoshiriki mashindano ya pikipiki kutoka mkoani Arusha wamekabidhiwa Bendera ya Taifa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenda kuiwakilisha Nchi kwenye mashindano ya Central African motocross challenge yatakayofanyika Vikingu, Mombasa Nchini Kenya.
Vijana hao ambao ni Lian Millar, Simon Vitalis, Collin Simonson, Caleb Simonson wakiongozwa na kocha Leenie Miller wataelekea kwenye masindano hayo yatakayofanyika tarehe 14 hadi 15 Desemba 2024.
Ikiwa ni mwendelezo wa kuibua vipaji kwa vijana wa Arusha, kuwapa fursa na kujipatia kipato, vijana hao ni matunda ya mashindano ya Samia Motocross Championship yaliyofanyika kwenye viwanja via Lakilaki tarehe 13-14 Julia, 2024 na hiyo ni mara ya pili kushiriki mashindano ya kmataifa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa