Na Elinipa Lupembe
Serikali ya awamu ya sita, imejipanga kuzipa makazi ya kudumu kaya zilizokosa makazi Kateshi, kufuatia maafa yaliyotokana na kumeguka sehemu ya mlima Hanang' kusababisha uharibifu wa mali na maisha ya watu
Ahadi hiyo, imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akizungumza na maelfu ya wakazi wa Kateshi, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Kateshi.
Katika Mkutano huo, Mhe. Rais, alitoa salama za pole kwa watanzania hususani wakazi wa Kateshi, walipoteza ndugu, jamaa na marafiki, majeruhi pamoja na wale waliokosa amakazi.
Mheshimiwa Rais, amesema kuwa zipo kaya takribani 440 zilizokosa makazi na kuthibitisna kuwa, Serikali imejipanga kuandaa eneo ambalo wataandaliwa makazi ya kudumu.
"Nimeagiza watalamu kufanya taarifa za uchunguzi wa kina, zinazohusu watu, mali na maeneo yote yaliyoathiri na kutafuta eneo, na bahati nzuri tumeshapata eneo ambalo watalamu litarasmishwa na Serikali ikifanya mpango wa kuwaandalia makazi ya kudumu ili waweze kuondoka kwenye makamazi ya muda" Amesema
Hata hivyo Mhe. Rais licha yakuwaapa pole wakazi wa Hana ng, amewashukuru na kuwapongeza kwa nidhamu na utulivu wa hali ya juu, walionyesha kipindi chote tangu maafa yaliopotekea na kuendelea kuomboleza kwa amani huku wakifuata maelekezo, waaliyopewa na viongozi wao wa dini, mila na Serikali.
Aidha, amewashuku watanzania wote makampuni, taasisi, mashirika, mikoa jirani, waliyotekeza waliowakimbilia wanakatesh nankutoa misaada ya hali na mali, ikiwemo vyakula, magodoro, mablanketi na huduma zote za msingi ambazo zilihitajika kwa haraka, na kuthibitisha kuwa, huo ndio kitendo hicho kimeonesha uzalendo, umoja na upendo miongoni mwa watanzania.
Akiwasiliisha taarifa ya maafa hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama, amesema kuwa, maafa hayo yamesababisha vifo vya watu 76 majeruhi 117, kaya 1,150 zenye watu 5,600 zikiathitika huku watu 440 zilizopoteza makazi na kuhifadhiwa kwenye kambi maalum za shule ya sekondari Kateshi na Ganana na shule ya msingi Genabi.
"Kwa maelekezo yako Mhe. Rais, serikali iligharamia mazishi ya marehemu 76 kwa kushirikiana na familia zao, na kutoa huduma zote ikiwemo malazi na chakula kwa kaya 1,150 zilizokosa makazi pamoja na kuwatibu majeruhi 117 waliolazwa kwenye vituo vya afya Kateshi na Babati"Amefafanua Mhe. Jenista
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, amemshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kutoa maelekezo ya haraka katika kukabiliana na Maafa hayo, maagizo ambayo yametekeelezwa na watalamu wake, na kuhakikisha wananchi wa Katesh, wanapata huduma stahiki licha ya kupoteza jamaa na mali zao.
"Ninakuaahidi watalamu wa sekta mbalimbali wataendelea kuweka kambi hapa Katesh, mpaka hali ya itakapokuwa shwari na kuhakikisha wananchi wanarejea na kuendelea na shughuli zao za kawaida, tunayo akiba ya chakula ya kutosha kuwahudumia wahanga na watalamu kwa muda wa mwezi mmoja" Waziri Mkuu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa