Wamiliki wa shule binafsi Mkoani Arusha wametakiwa kuhakikisha wanafuata miongozi na taratibu za uwendeshaji wa shule zao hasa zinazotolewa na Wizara ya Elimu na TAMISEMI.
Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta alipokuwa akifungua kikao cha kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2021.
Amesema kitenda cha baadhi ya shule kufutiwa matokea kwasababu ya udanganyifu uliofanyika katika shule hizo ni kitendo cha aibu sana na kinarudisha maendeleo ya ufaulu nyuma.
“Ninakilaani sana kitendo hiki cha baadhi ya shule kufanya udanganyifu katika mitihani na kupelekea wanafunzi kufutiwa matokea, wakati wazazi wamelipa ada kwa ajili ya watoto wao.
Mhe. Kimanta amewataka wamiliki wa shule hizo kuwa waaminifu kwa kuongeza juhudi za ufundishaji ili waweze kupata matokea mazuri na halali.
Akisoma taarifu fupi ya matokeo hayo Kaimu Afisa Elimu Mkoa bwana Emmanuel Maundo amesema, jumla ya wanafunzi 40,729 walisajiliwa kufanya mtihani na 37,057 ndio waliofaulu sawa na asilimia 92.42.
Ufaulu huo ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 2,548 sawa na asilimia 0.75 kulinganisha na mwaka 2019 ambapo ufaulu ulikuwa ni asilimia 91.67.
Bwana Maundo amesema, kutokana na ufaulu huo kumepelekea hata uhitaji wa miundo mbinu ya shule kuongezeka kama madarasa, madawati, viti na meza na matundu ya choo.
Mkoa wa Arusha umeshika nafasi ya pili Kitaifa katika matokea ya darasa la saba kwa mwaka 2020.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa