Na Prisca Libaga
Serikali kupitia Tume ya Mipango imewapa Wanamipango, mwelekeo wa Serikali katika utekelezaji wa majukumu katika kupanga mipango kwenye maeneo yao za kazi, ili kufikia malengo ya
Serikali imewapa mwelekeo huo,wakati wa Kongamano la Wanamipango , uliowakutanisha Maafisa Mipango kutoka Wizara zote, Idara za Serikali zinazojitegemea, Mashirika ya Umma pamoja na Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Akizungumza na Wanamipango hao, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru, amesema kuwa Kongamano hilo, pamoja na kuwapa Wanamipango nafasi ya kufahamiana na kubadilishana uzoefu, lina lengo la kuwanoa ili kiwa na uelewa wa pamoja, mwelekeo wa Serikali na Matarajio yake, kupiti mada mbalimbali, zitakazowasilishwa kwenye Kongamano hilo.
Amesema kuwa, kutokana na kuundwa kwa Tume ya Mipango na matakwa ya kisheria kwamba, Tume hiyo itakuwa mratibu na msimamizi mkuu wa kada hiyo ya Wanamipango, hivyo, Tume kutumia Kongamano hilo, kuwakumbusha majukumu yao na kuendana na zama mpya za upangaji wa shughuli za maendeleo.
“Serikali inatekeleza majukumu yake kwa kupanga na kila jambo linaanzia kwenye Idara ya Mipango, tunashukuru tumeweza kuwaleta pamoja wanamipango wote wa Serikali, hapa tutapata nafasi ya kufanya tathimini ya changamoto tulizonazo na kwa kuwa sisi ni wapangaji tuanze pia kutafuta majawabu ya changamoto hizo,”alisema Mafuru.
Katika Kongamano hilo la kwanza baada ya Serikali Kurejesha Wizara ya Mipango, zaidi ya Wanamipango 400, wamehudhuria kongamano hilo, linalofanyika Mkoani Arusha, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), likiongozwa na Kaulimbiu ya ‘Fikra za Pamoja na Utekelezaji Uliratibiwa kwa Ustawi Jumuishi’.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa