Wananchi mbalimbali wamejitokeza kupata msaada wa kisheria bure kwenye banda la Wizara ya Katiba na Sheria ikiwa ni siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, kuelekea kilele Machi 08, 2025.
Katika Maadhimisho hayo huduma za kijamii zitatolewa bure ikiwemo huduma za afya, msaada wa kisheria huku Wizara nane zikijikita kwenye utoaji wa huduma bure.
Mgeni Rasmi kwenye Kilele cha Siku ya Wanawake2025 ni Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Kauli Mbiu: Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji
Tukutane Arusha, kuanzia Machi 01, Usipange Kukosa
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.