Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola ameagiza jeshi la Polisi kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha watu wote watakaotumia mitandao ya kijamii kukashifu Mtu au nchi wakamatwe na kufunguliwa kesi kwa mujibu wa sheria za mawasiliano nchini.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kubaini kuwa kuna baadhi ya Watanzania wanaikashifu nchi pamoja na Rais John Magufuli kwenye mitandao ya Kijamii na vyombo mbalimbali vya habari.
Lugola amesema hali hiyo inapelekea kujenga picha mbaya ya nchi ya Tanzania kuwa haina amani na utulivu lakini uhalisi hauko hivyo, kwani nchi imejaa amani na utulivu kila mahali.
Amesema serikali haita kaa kimya kabisa kwa mtu yoyote atakae toa maneno ya uwongo ili kuvunja amani ya nchi kwani nchi inasheria na taratibu hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa wote watakao toa maneno ya uchochezo na ya kuvunja amani nchi.
Aidha, amesema hali ya amtukioya uhalifu imepungua kutoka matukio 596,533 kwa mwaka 2017 hadi 591,803 kwa mwaka 2018 yani pungufu ya matukio 4,730 sawa na asilimia 0.8.
Pia, matukio makubwa na madogo ya barabarani kwa mwaka 2017 yalikuwa 2,522,998 na 2018 yalikuwa 2,722,720, hii ni ongezeko la matukio 199,722 sawa na asilimia 7.9 na hii imesababishwa na udhibiti na ukaguzi unaofanywa na jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani hapa nchini.
Kutokana na hali hii Mhe. Lugola amewaondoa shaka wageni wote hasa watalii na wawekezaji kuwa hali ya usalama kwa nchi ya Tanzania ni nzuri sana naya utulivu.
Mhe. Kangi Lugola yupo ziarani Mkoani Arusha kuzungukia Wilaya zote za Mkoa huu ambapo atakutana na kufanya vikao na kamati za ulinzi na usalama za wilaya na pia atazungumza na kamati za chama cha Mapinduzi kwa lengo lakuona ni kwa namna gani ilani ya chama imetekelezwa hususani upande wa ulinzi na usalama.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa