• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WATENDAJI WA KATA WAMETAKIWA KUZIFAHAMU BAJETI NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZOTE  ZA MAENDELEO KWENYE KATA ZAO

Posted on: June 4th, 2024

Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, amewaagiza Maofisa Watendaji wa Kata zote za Mkoa wa Arusha kufahamu bajeti ya mapato na matumizi ya Kata husika kwa mwaka mzima.

Mhe. Makonda ametoa agizo hilo wakati akisikiliza kero na changamoto za wananchi wa Kata ya Mateves, kufuatia agizo la Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi la kumtaka kurudi kata ya Mateves ili kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi hao, ambapo Mhe. Makonda amerudi leo mapema  Juni 04, 2024.

Mhe. Makonda amewaagiza Maofisa hao kuhakikisha wanazifahamu vema bajeti na mipango ya kata zao kwa mwaka husika pamoja na utekelezaji wa shughuli na miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwenye kata husika huku wakifahamu muda wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Amefafanua kuwa, kila Mtendaji anatakiwa kufahamu aina ya miradi iliyotekelezwa kwenye kata husika na gharama zake kisekta huku mikataba ya miradi hiyo, kiasi cha fedha alicholipwa mkandarasi na wazabuni waliotekeleza miradi, idadi ya wanufaika wa miradi hiyo pamoja na tija ya miradi kwa wanufaika.

"Ninakerwa na uwajibikaji na ufanisi mdogo wa baadhi wa watendaji wa Serikali za mitaa na vijiji, baadhi yao wamekosa sifa za kuwatumikia wananchi kutokana na uwajibikaji mdogo kwenye vituo vyao vya kazi, unaosababisha kero na malalamiko mengi kwa wananchi na kuichukia Serikali" Amebainisha Mhe.Makonda.


Hata hivyo Mhe. Makonda ameahidi kuanza kufanya ziara ya kata kwa kata mkoani Arusha na kuwataka Maofisa hao wa kata kujiandaa kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli wa maendeleo za kata zao wakati wa ziara hiyo maalum ya kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi. 

#ArushaNaUtalii

#kaziinaendelea

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa