Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha, wakimkabidhi zawadi kama ishara ya upendo, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Albano Musa.
Watumishi hao wamemuelezea Katibu Tawala huyo, kuwa ni kiongozi anayewapa na kuwakusanya pamoja watumishi hao kama baba na sio 'boss', asiyebagua watoto wake, jambo linalojenga umoja na ushirikiano, ukiwapa nguvu ya kufanya kazi kama timu na kuufanya eneo la kazi kuwa ni ofisi salama katika utumishi wao
Wamethibitisha kuwa, upole, busara na hekima alizojaliwa kiongozi huyo, zinawapa nguvu watumishi kufanya kazi kwa bidii na weledi huku wakiweka uzalendo mbele kila mtumishi na fani yake kwa kuithamini dhamana waliyopewa na Serikali yao ya awamu ya sita chini ya mheshiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo, watumishi hao wamemuombea Mwenyezi Mungu amjalie baraka na maisha marefu na afya njema, ili aendelee kuwasimamia watumishi hao.
Watumishi hao, wempongeza Kiongozi huyo, wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2024, iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha, ukumbi wa Nyasa, Jijini Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa