• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WAWEKEZAJI ARUSHA WAPONGEZA SERA BORA ZA UWEKEZAJI NCHINI..

Posted on: January 16th, 2024


Na Elinipa Lupembe

Wawekezaji wa Kampuni ya  Hanspaul inayomiliki Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari maalum kwa ajili ya shughuli za Utalii  mkoani Arusha, wameipongeza na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwa na Sera bora zinazovutia wadau kuwekeza nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Hanspaul, Satbir Singh Hanspaul kiwandani hapo, hakusita kuipongeza Serikali,  kwa kuwa na Sera nzuri zinazosababisha mazingira rafiki kwa wawekezaji kufanya kazi za uzalishaji nchini. 

Ameweka wazi kuwa, kupitia Kituo cha Uwekezaji cha Taifa,  imeweka mazingira rafiki yanayowezesha wawekezaji wa ndani kufanyakazi kwa kushirikiana na sekta zote, zaidi mazingira yanayoruhusu na kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi kuwekeza Tanzania.

"Kiwanda chetu tunatengeneza magari yanayotumia umeme na yameanza kutumiwa na watalii, tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Tamthilia ya Royal Tour imeleta watalii wengi nchini, watalii ambao baaadhi yao wanavutiwa kuwekeza Tanzania, huku TIC ikifanyakazi kubwa ya kuwaunganisha wafanyabiashara wakubwa, makampuni na watu binafsi".Amesema Satbir Singh

Hata hivyo amesema kuwa kutokana na amani na utulivu  wa kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini, umewezesha watanzania na wageni kutoka nje ya nchi kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa uhuru, unaokwenda sambamba na kukuza uchumi wa nchi.

Awali, Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Felix John amesema kuwa, TIC inafanya kampeni ya kitaifa kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani, ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu zana ya uwekezajia pamoja ja kubadili fikra na mtazamo wa watanzania kwamba wawekezaji ni wageni kutoka nje ya nchi.

"Kampeni hiyo ni muhimu kwa watanzania, inayolenga pia kuwahamasisha watanzania,  kushiriki kikamilifu kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na kuchangamkia fursa zilizoko" Amebainisha John

Hata hivyo, ameaeka wazi kuwa, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, kwa kushirikiana na TIC, wameshusha kiwango cha fedha za uwekezaji hasa kwa wazawa kutoka Dola za Kimarekani 100,000 hadi kufikia 50,000 sawa na Sh.milioni 125, kwa lengo la kuwavutiwa wawekezaji wa ndani kuwekeza na kusajili miradi.

#arushafursalukuki




                        
                       
                        </div>
                        <!-- /.right-sidebar-content -->
                        <!--/END RIGHT SIDEBAR CONTENTE SECTION-->
                    </div>



<div class=

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa