• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

ZOEZI LA KUWAPANGA MACHINGA KUANZA NOVEMBA 1,2021

Posted on: October 30th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella ametangaza rasmi zoezi la kuanza kuwahamisha machinga kuanza Novemba 1,2021 hadi Novemba 3,2021 Jijini Arusha.

Ameyasema hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa masoko hayo yaliyopo Engutoto Njiro, soko la Mbauda,eneo la Machame Luxury, eneo la Ulezi na kiwanja namba 68 Kilombero.

"Zoezi la kuwapeleka machinga katika maeneo yao ya masoko mapya katika Jiji la Arusha litakuwa la utulivu na utaratibu unaoeleweka",alisema.

Aidha, amesema kinachotakiwa ni ushirikiano kwa watu wote na zoezi litakuwa rahisi na la amani.

Mongella amesema katika hali ya kuliweka Jiji la Arusha nadhifu na la kuvutia wamachinga hao watapangwa kulingana na aina ya bidhaa wanazouza.

Amesema Soko la Engutoto litakuwa maalumu kwa bidhaa za thamani tu na wahusika ndio watajenga wenyewe mabanda yao.

Alikadharika soko la Mbauda litakuwa la nguo za mitumba, soko la Machame litakuwa la vyombo na vifaa vya umeme, soko la Ulezi litakuwa maalumu kwa nguo za dukani na soko la Kilombero kiwanja namba 68 litauza mbogamboga na Matunda tu.

Mongella amewataka wamachinga wote kutumia hizo siku 3 alizotoa kuhamia katika masoko hayo kwa utaratibu utakaokuwa unatangazwa na magari ya Serikali.

Pia, amewataka wafanyabiashara wa maduka kurudisha bidhaa zao ndani ya maduka kwani baadhi yao walitoa nje ya maduka ili kutafuta wateja kupitia kwa machinga hao.

Vile vile amewataka wafanyabiashara katika soko ya Kilombero na soko Kuu kuhakikisha wanakaa kwenye meza zao na kulipa kodi  kulingana na makubaliano yaliyopo na Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Ametahazalisha kwa watakaoshindwa kurudi katika maduka na meza zao katika masoko hayo basi watapewa wafanyabiashara wengine waliokosa maeneo.

Amesema faida kubwa ya kuwapanga wamachinga ni kuliweka Jiji katika mpangilio unaovutia kwani ni mji wa kitalii lakini pia utasaidia wamachinga kutambulika na Serikali kwa urahisi na hivyo kuwa na fursa rahisi ya kupewa mikopo ya Halmashauri.

Nae, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. John Pima amewataka wafanyabiashara wote waliokimbia vibanda na meza zao katika masoko kufikia Novemba 1,2021 wawe wamerudi katika maeneo yao na ukaguzi utafanyika siku hiyo.

Amesema kila machinga atakaepewa kibanda atapewa kitambulisha cha machinga cha Jiji ili watambulika kirahisi.

Mwenyekiti wa wamachinga Mkoa wa Arusha Bi. Amina Njoka amewataka wamachinga wote watulie wakisubiri maelekezo ya namna zoezi hilo la kuwapanga katika maeneno yao litakavyofanyika.

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wamachinga hao na kuwawekea  utaratibu mzuri wa ufanyaji biashara utakaowafanya watambulike na kunufaika nao.

Zoezi hilo la kuwapanga machinga limetangazwa rasmi kuanza Novemba 1 hadi Novemba 3 ikiwa ni maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan Septemba 13, 2021 na kusisitizwa zaidi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mnamo septemba 15, 2021.



Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa