Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengera amewaongoza wakazi wa Arusha kuadhimisha Miaka 60 ya Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi kwenye Hosptali ya Jiji la Arusha eneo la Njiro leo Aprili 26, 2024
Katika Maadhimihso hayo, licha ya kupanda miti na usafi wa mazingi, wananchi walijitokeza kwenye zoezi la uchangiaji damu Salama.
Hata hivyo, Mkuu huyo wa wilaya amewataka watanzania wote kuuenzi Muungano kwa kuhakikisha kila mtu anaifahamu historia ya Muungano na kudumisha amani, upendo na mshikamano huku akiweka mbele utaifa pamoja na kurithisa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Kauli mbiu; " Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano, Tumeshikamana na Tumeimarika kwa maendeleo ya taifa letu."
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.