Na. Elinipa Lupembe
Mkuu wa mko wa Arusha Mhe.John V.K Mongella, amesema Hayati Edward Lowassa atakumbukwa na wakazi wa mkoa wa Arusha kutokana na uzalendo na uchapakazi wake, ambao umechangia maendeleo na mafanikia ya mkoa wa Arusha
Mhe. Mongella ameyasema hayo, wakati akitoa salamu za Mkoa wa Arusha, kwenye ibada Maalum ya Shukrani ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowasa, iliyofanyika kwenye kanisa la KKKT Usharika wa Monduli Leo Machi, 24, 2024.
Amesema kuwa, Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Arusha, Hayati Edward Ngoyai Lowassa ataendelea kukumbukwa kwa mambo makubwa aliyoyafanya mkoani Arusha, ikiwa ni pamoja na mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya mkoa na wananchi wa mkoa wa Arusha.
"Kwa niaba ya wananchi wa Mkao wa Arusha, tutaendelea kuyaenzi maisha ya mzee Lowassa, kwa kazi kubwa aliyoifanya katika mkoa wa Arusha, na tutaendelea kushirikiana na familia mama na watoto". Ameweka wazi Mhe.Mongella.
Aidha, ameishukuru familia kwa kuwakaribisha kwenye ibada hiyo muhimu, licha ya kutoa pole kwa familia amewataka wanafamilia kuendelea kumtegemea Mungu
Awali, familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa imeandaa ibaada ya shukrani, kwenye kanisa la KKKT Usharika Monduli, inaada iliyoongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazin Kati, Mchungaji Lareton Loishiye.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.