Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amesema matumizi ya dira za malipo ya kabla ya maji si kwa wale wateja sugu wasiolipa madeni bali ni kwa wateja wote wa huduma ya maji.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua kwa mala ya kwanza huduma hiyo kwa mkoa wa Arusha katika ofisi ya mkuu wa mkoa.
“Watu wengi wanadhani huduma hii ni kwa wateja wasiopenda kulipa bili za maji, hapana huduma hii ni kwa wateja wote wanaopata huduma ya maji kutoka mamlaka ya maji safi na taka”.
Malipo ya maji ya kabla yatasaidia sana kuongeza mapato na pia itasaidia kuondoa malalamiko yaliyokuwa yanatolewa na wateja wetu kulipa bili kubwa kuliko matumizi yao.
Lengo letu nikuhakikisha wateja wetu wanapata huduma nzuri,bora na kwa wakati kwasababu ya ukuwaji wa hii teknolojia na hata wale wateja sugu wasiopenda kulipa watalipa kupia huduma hii..
Akitoa shukrani zake kwa Waziri Mbarawa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema amefurai kwa huduma hiyo mpya kuanza kutumika rasmi kwa mkoa wa Arusha na hasa katika ofisi yake.
Amesema atazisimamia taasisi zote za serikali zilizopo katika mkoa wa Arusha kuanza kutumia huduma hii mara moja bila kuchelewa na ataendelea kuiunga mkono kwa mkoa mzima.
Huduma ya malipo kabla ya maji ilizinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam na inaendelea kusambazwa katika mikoa mingine nchini.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.