Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha wamewapongeza wananchi wa kata ya Seela Singisi, kwa ushirikiano wao uliofanikisha kukamilisha ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Madiira, shule ambayo imejengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 584.2 kupitia program ya SEQUIP.
Wajumbe hao wa Kamati ya Siasa wametoa ponhezinhizo mara baada ya kutembelea shuleni hapo na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa shule hiyo, shule ambayo tayari imekamilika na wanafunzi wameanza masomo shuleni hapo tangu muhula mpya wa masomo wa mwaka 2024 ulipoanza mapema Januari 08 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati, Loy Thomas Ole Sabaya, amewaponheza wananchi hao kwa kushiriki usimamizi wa mradi huo, ambao umekamilika ukiwa na viwango vya ubora unaoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Aidha ameupongeza uongozi wa mkoa, wilaya na halmashauri kupitia watalamu wasimamizi wa mradi, kwa namna wamesimamia vema utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020 - 2025 kupitia mradi huo na shughuli zote zinazofanyika kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
"Mmefanya kazi nzuri mnastahili pongezi, tayari wanafunzi wameanza masomo, lakini mmepanda miti kuzunguka mazingira yote ya shule, mazingira ni mazuri yanavutia kusoma, niwasihi walimu na wazazi kuwasimamia watoto hawa kusoma ili kufikia lengo la Serikali ya awamu ya sita ya kupata watalamu wa fani mbalimbali watakaokuja kulitumikia Taifa la Tanzania" Amesema Sabaya.
Awali Kamati hiyo ya Siasa imafanya ziara ya kawaida ya kukagua miradi ya Maendeleo halmasahuri ya Meru, ikiwa ni ukaguzi wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020 - 2025.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.