Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa - NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndugu, Paul Christian Makonda, amewasili mkoani Arusha akitokea mkoa wa Kilimanjaro na kupokelewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Ndugu Loy Thomas Ole Sabaya, pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali wa mkoo huo, eneo la King'ori, wilaya ya Arumeru, leo Januari, 23, 2024.
Akiwa mkoani Arusha, Ndugu Makonda atafanya ziara ya siku mbili, pamoja na shughuli nyingine za Kichama, atafanya Mikutano ya hadhara katika wilaya tatu za mkoa wa Arusha.
Siku ya kwanza ya ziara hiyo, atazindua tawi la Wakereketwa la Usa River, na kufanya Mkutano wa hadhara eneo hilo la Usa River katika wilaya ya Arumeru, na baadaye kukutana na Kamati ya Siasa mkoa na kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama mkoa pamoja na kukutana na Wazee waasisi, viongozi wa dini na mila pamoja na wakuu wa Taasisi, mikutano itakayofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano CCM Mkoa wa Arusha.
Aidha atafungua tawi la wakereketwa eneo la Kilombero na baadaye kufanya Mkutano wa hadhara eneo hilo la Kilombero katika wilaya ya Arusha.
Siku ya pili ya ziara yake atafanya mkutano wa hadhara eneo la Makuyuni wilaya ya Monduli.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.