Muuguzi Mkuu na Mratibu wa M-mama Mkoa wa Arusha, Getrude Anderson akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa mfumo wa m-mama mkoa wa Arusha kwenye kikao kazi cha mwaka cha Tathmini ya utekelezaji wa mfumo wa huduma ya M - mama mkoa wa Arusha, kilichofanyika kwenye hoteli ya Corridor Spring Jijini Arusha mapema leo Julai 30, 2024.
Amesema kuwa, Mfumo wa m-mama ni mfumo wa usafiri na rufaa ya dharura kwa wajawazito na watoto ambapo mkoani Arusha ulizinduliwa mwezi Desemba, 2022 na tekelezaji wake ulianza rasmi Machi, 2023.
Kwa tathmini ya jumla kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitatu mkoa wa arusha umefanya vizuri kwa kufikia asilimia 92 kwa kusafirisha wagonjwa 5, 069 mkakati ambao umesaidi kupunguza vifo 19 kutoka vifo 64 na kufika vifo 48 sawa na asilimia 28.3 huku mkoa ukiwa na mkakati wa kufikia vifo sifuri.
Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kuimarisha na kuboresha vituo vinavyotoa huduma za Afya ya mama na mtoto huku mkoa wa Arusha ukitumia mfumo wa m- mama ambao umekuja kurahisisha kupunguza vifo vilivyotokana na kukosekana kwa usafiri kwa wajawazito wakati wa kujifungua pamoja na usafiri wa dharura kwa kupiga namba 115
"Awali tulianza kwa kusafirisha wajawazito kutoka kwenye vituo vya afya na sasa tunaanza kusafirisha kutoka kwenye jamii kwenda kwenye kituo vya afya, huku jamii ikiendelea kupewa mafunzo ya huduma muhimu ya m-mama " Amesem Getrude
Aidha, amesema licha ya mafanikio makubwa bado kuna changamoto za uelewa wa jamii pamoja na baadhi ya Halmashauri kushindwa kuwalipa madereva kwa wakati, na kuzitaka halmashauri kuweka mpango mkakati wa kuwalipa maderva hao kwa wakati pamoja na kukaa vikao na madereva kwa kurejea mikataba na kuwapa elimu zaidi.
Wananchi wanatakiwa kutumia namba 115 kwa ajili ya huduma za m- mama huduma ambayo tayari Serikali imeshalipia gharama za usafiri kwa wajawazito kutoka kwenye maeneo yao na kufikia kwenye kituo cha karibu cha kutolea huduma za afya na hata pindi atakapohitajika kwenda kwenye hospitali ya Rufaa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.