Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava ametembelea na kukagua mradi wa uwezeshaji vijana Kiuchumi Kikundi cha Vijana cha Agri - Genius, mradi wenye thamani ya shillings milioni 32.
Mradi huo wa vijana, waliopata mkopo wa shilingi milioni 30 kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Vijana, wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji na mazao cha mbogamboga na matunda, walianza mradi huo kwa shilingi milioni 2.
Katika mradi huo, Ndugu, Mnzava licha ya kuridhishwa na shughuli zinazofanywa na vijana hao, amewapongeza kwa kuwa wazalendo wa kulitumikia Taifa lao na kuwataka kuongeza juhudi katika kazi zao na kuwa mfano na vijana wengine.
"Taifa letu linawategemea vijana katika kusukuma gurudumu la amendelea, nyie ni vijana wa mfano, kazi mnazozifanya wahimizeni na vijana wenzenu kufanyakazi hasa za kujiajiri" Amesema Mnzava.
Aidha amewaagiza Maafisa Maemdeleo ya Jamii na Maafisa Biashara kuwasaidia vijana wanaojiajiri katika shughuli za kilimo kuondolewa vikwazo pale wanaposafirisha mazao yao ndani na nje ya nchi kama kuna vibali wapewe mapema ili waweze kufanya shughuli zao kwa urahisi ili biashara zao ziweze kuwa za kimataifa na kupiga hatua zaidi.
"Niwasihi vijana kuacha kukaa vijiweni badala yake kujiajiri kwa kubuni biashara ndogondogo ili kutumia fursa ya kupata mikopo isiyo na riba na ile ya Ofisi ya Waziri Mkuu inayotolewa na Serikali, Serikali ina mikakati ya kuwawezesha vijana kiucbumi hivyo vijana acheni kulalamika tumieni fursa hizo kujiajiri" Amesema
Akisoma taarifa ya mradi huo, Mwenyekiti wa Kikundi, Godfrey Rogath, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mkakati imara wa kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kutoa mikopo ambayo inawapa fursa vijana kujiajiri na kujiinua kiuchumi.
"Mkopo huu umetuwezesha kuongeza mtaji wetu kutoka milioni 2 na kufikia milioni 32 mpaka sasa, baada y kupata mkopo wa milioni 32, tumeweza kujenga kitalu nyumba, kuongeza eneo la kilimo kutoka heka 1 na kufikia Heka 4"
Ameongeza kuwa Mkopo huo umewawezesha vijana kujiajiri na kuweza kujipatia kipato na kuajiri vijana wengine na kuwa mfano kwa vijanza wenzao wanaokuja kujifunza shughuli za kilimo.
Awali kikundi hicho chenye wanachama watano kilinza mwaka 2022 na kusajiliwa kwa namba ARU/ ARU/VIJ/2022/20247.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.