Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa, Loy Thomas Ole Sabaya, amewasIsitiza wanafunzi kutumia fusa waliyonayo kusoma kwa bidii na kujikita zaidi kwenye masomo, kwa kuwa tayari Serikali yao, imewaandalia mazingira mazuri na rafiki ya kujisomea.
Mwenyekiti Sabaya ametoa wito huo, alipozungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Nasholi, halmashauri ya Meru, wilaya ya Arumeru, wakati Kamati ya Siasa ilipofanya ziara ya Kukagua miradi ya Maendeleo katika halmshauri hiyo, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020 - 2023 mkoa wa Arusha kuanzia mwezi Julai - Desemba, 2023.
Amefafanunua kuwa, Serikali ya Awamu ya sita, imefanyakazi kubwa na kuwekeza fedha nyingi katika kujenga na kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu, hivyo ni jukumu la wanafunzi sasa kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao, lakini zaidi kupata ujuzi na maarifa yatakayowawezesha kulitumikia Taifa hapo baadaye.
"Serikali ya mama Samia, imewajengea shule nzuri, tumieni fursa hii adhimu kusoma, msidanganyike na kuacha shule, hakikisha unaelekeza akili zote kwenye masomo ili kufikia ndoto zenu, wapo waliosema wanataka kuwa madaktari, wahandisi, walimu, hakikisheni mnafika vyuo vikuu" Amesema Sabaya.
Hata hivyo, amewataka walimu na wazazi kushirikiana kuwasimamia watoto ili waweze kuhitimu masomo yao kama kufikia malengo ya Serikali ya kuhakikisha watoto waote wakitanzania wanapata elimu.
Aidha amewasisitiza wazazi kuhakikisha wanawapa watoto wao, mahitaji yote ya Msingi ikiwemo kuwa na utaratibu wa kuwapa watoto chakula cha mchana wawapo shuleni.
Awali, mradi huo wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi Nasholi, imejengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 348.5 kupitia programu ya kuboresha miundombinu ya shule za Msingi Tanzania Bara (SEQUIP).
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.