• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

NAIBU WAZIRI KATAMBI APONGEZA HALI YA UTOAJI HUDUMA KITUO CHA HUDUMA ZA PAMOJA (OSBP) NAMANGA....

Posted on: January 3rd, 2024


Na Elinipa Lupembe.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Pascal Katambi Patrobass (Mb), ameridhishwa na hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma  kwa wasafiri wanaopitia mpaka wa Tanzania na Kenya kupitia Kituo cha Huduma za pamoja Mpakani (OSBP), eneo la Namang na kuwapongeza watendaji wa kituo hicho chenye ofisi za Taasisi 18 muhimu, ambazo ni maalum kwa kuwahudumia wasafiri wanaovuka mpaka huo.

Mhe. Katambi amesema hayo wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kukagua na kujionea hali halisi ya utendaji kazi na utoaji huduma katika mpaka huo kwa wasafiri, mali na mizigo yao pamoja na magari ya mizigo na kupongeza namna Serikali imeweka mifumo rahisi ya kudhibiti upitaji wa abiria na mizigo lakini kuwarahisishia wasafiri upatikanaji wa vibali vya kuvuka katika eneo moja.

Amesema kuwa, licha ya Kituo cha pamoja kuwa na mifumo inayowarahisishia abiria kupita mpakani, lakini amewataka wataalam kuzingatia hali ya usalama katika mipaka kwa kufanya upekuzi wa abiria na mizigo yao pamoja na magari ya mizigo kwa umakini na kujiridhisha, raia wanaovuka mpaka huo wanavyo vibali vyote halali ili kuzuia uhamiaji haramu na upitishaji wa bidhaa za magendo.

"Nimejionea Mifumo bora ya kuhudumia wasafiri inayodhibiti watu kupita bila vibali muhimu, ninaona uwepo wa miundombinu rafiki yenye mifumo ya kisasa, unaruhusu kila abiria kukaguliwa na kulipia na kupata vibali vyote katika eneo moja pamoja na kudhibiti usafirishaji haramu wa mali na binadamu, kituo ambacho kina hadhi ya kimataifa, ni ngumu sana mhalifu kupita hapa" Ameweka wazi Mhe. Katambi

Naye Mfawidhi wa Uhamiaji mpaka wa Namanga, Mrakibu wa Uhamiaji Bulugu Edward Mkanga, amesema kuwa, kituo hicho kinazo ofisi 18 za taasisi zinazohusika na usafiri wa mpakani na kuongeza kuwa makubaliano ya 'communique' yanayoruhusu raia wa nchi hizo mbili kutembea hadi Km 20 kwa pande zote umepunguza uhalifu na kuongeza muingiliano wa amani wa kijamii na kibiashara katika eneo la Tanzania.

"Kupitia 'communigue' raia wa Kenya anaruhusiwa kuingia hadi kipenyo cha Km 20 katika eneo la Tanzania kadhalika na raia wa Tanzania anaruhusiwa kuingi Kenya kipenyo hichohicho bila ya kuwa na kibali chochote, zaidi ni kitambulisho cha utaifa tu,  jambo ambalo limefanikiwa kuongeza muingiliano wa kibiashara mpakani huku Tanzania ikinufaika kutoka na raia wengi wa Kenya kupenda kufika kuja eneo la Tanzania hasa nyakati za weekend kupata huduma za burudani" Amesema Mkaribu wa Uhamiaji Mkanga.

Hata hivyo, Mkuu wa wilaya ya Longido, Mhe. Marco Ng'umbi, amesema kuwa, hali ya usalama wilayani hapo ni shwari huku wakazi wake wakiendelea na shughuli zao za kila siku za kujitafutia kapato kwa kuzingatia taratibu na sheria za nchi, licha ya makubaliano ya muingiliano huo wa kipenyo cha kuingia hadi Km 20 kwa raia wa mpakani kwa pande zote mbili.

"Wilaya ya Longido inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kusimamia matumizi ya mifumo inayotumika kwenye kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani (OSBP) Namanga, na kuhakikisha raia wanaoingia na kutoka nchini wanafuata taratibu zote, huku kukiwa na utaraibu imara na thabiti wa ukaguzi wa magari madogo na magari ya mzigo kabla ya kuvuka na kuingia nchini" Amefafanua Mhe. Ng'umbi

#arushafursaluki




Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.