NENDENI MKAWEKEZE KATIKA FEDHA ZA TASAF ILI ZIWAINUE KIUCHUMI.
Wanufaika wa fedha za TASAF wametakiwa kutumia fedha hizo katika kuzalisha ili wakuze uchumi wa kaya zao.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF)Mkoa wa Arusha bwana Richard Nkini alipokuwa akikagua zoezi la ugawaji wa fedha kwa wahitaji wa Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha.
" Lengo la TASAF ni kuinua uchumi wa kaya husika hivyo nawasii walengwa wote hakikisheni mnapopata fedha hizi mkawekeze kwenye miradi mbalimbali kama vile ufugaji".
Bwana Nkini amesema TASAF inatoa fursa kubwa kwa wananchi kuweza kuendesha maisha kwa kulipa ada, kununua chakula,kujenga nyumba za kuishi na kufuga.
Aidha, amewataka waratibu wa TASAF ngazi ya halmshauri kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha hizo kwa wananchi ili mpango huu uweze kuwanufaisha zaidi walengwa kiuchumi.
Nae,Uchumi wa Mkoa bwana Jonath Mwita amesisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya fedha za TASAF ili wanufaika waweze kujikwamua kiuchumi na kutoka katika hali ya umaskini.
Mtendaji wa kata ya Olmotonyi kutoka halmashauri ya Arusha bwana Epimack Nyampanda amesema bado kuna waitaji wengi wa fedha hizo katika kata yake.
Zoezi la ukaguzi wa miradi na utoaji wa fedha za TASAF ngazi ya Mkoa awamu ya tatu katika kipindi cha 2 linaendelea katika halmashauri zote na Mkoa umepata fedha zaidi ya bilioni 2 kwaajili ya walengwa 58,309 wanaotoka katika vijiji 587.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.