Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Arusha leo Agosti 27, 2024 kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro na kupokelewa na Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu. Mhe. Rais Samia amepangiwa kufungua Kikaokazi cha Wenyeviti wa bodi na Watendaji wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za serikali (CEO's FORUM 2024) Mkutano unaofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC Jijini Arusha.
Kikaokazi hicho kinachozinduliwa jumatano hii Agosti 28, 2023, kina lengo la kuwafahamisha na kuwashirikisha maafisa hao juu ya maboresho yanayoendelea katika kuimarisha usimamizi, uendeshaji na utendaji wa Taasisi za umma sambamba na kubadilishana uzoefu kwa watendaji hao.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.