Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amezindua na kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 03, 2023 Hanang, hafla iliyofanyika kwenye kijiji cha Wareti, Wilaya ya Hanan'g mkoani Manyara mapema leo Desemba 20, 2024.
Nyumba hizo ambazo zimejengwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Samia Suluhu Kwanza kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT).
Hatahivyo nyumba hizo zimejengwa kufuatia ahadi na maamuzi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na maporomoko ya tope na kujionea uharibifu mkubwa uliotokana na maparomoko hayo, huku zaidi ya watu 700 wakipoteza ndugu, mali na hata makazi.
Uamuzi huo ni muendelezo wa dhamira ya dhati ya Serikali ya kuwalinda na kuwahudumia wananchi wake na kurejesha matumaini ili waendelee na mfumo wa kawaida wa maisha baada ya maafa hayo kutokea.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.