Theresia Sabore Moko, aliyekuwa mkazi wa kata ya Enduleleni, wilaya ya Ngorongoro, akizungumza kwa niaba ya wanawake walioamua kuama kwa hiari na kupisha eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, wakati wa hafla fupi ya kuagana, iliyofanyika kwenye Ofisi za zamani za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro leo tarehe 25 Januari, 2024.
Theresia amempongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuziandalia familia zao makazi mapya nje ya eneo lHifadhi, eneo ambalo familia mara kwa mara zilikumbwa na changamoto ya kujeruhiwa na wanyama, na wengine walipoteza maisha kwa kushambuliwa na wanyama.
"Mimi na familia yangu, tumeamua kujiandikisha kwa hiari, kuhamia Msomera, eneo ambalo Serikali imetupa bure bila kutoa gharama yoyote, tumeona ni eneo salama kwa maisha yetu na familia, zaidi tumeamua kuanza maisha mapya na kuanza kufanya shughuli za uzalishaji mali, shughuli ambazo tukiwa ndani ya Hifadhi hatukuruhusiwa kuzifanya kama vile kilimo" Amebainisha Theresia
Ameipongeza Serikali kupitia watalamu wake kwa kuwapa elimu, iliyowawezesha kufanya maamuzi sahihi kwa faida yao na watanzania wengine ili Hifadhi hiyo ya Ngorongoro iweze kutunzwa na kubaki kwenye uhalisia wake kwa urithi wa vizazi hivi na vijavyo.
Ameongeza kuwa, walejiridhisha na eneo la Msomera wanalokwenda kuhamiq kwamba Serikali imejenga mindombinu yote muhimu ikiwemo ya afya na elimu, ambayo wana uhakikia watoto wao watapata elimu kwa uhuru.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.