Kukamilika kwa jengo la utawala la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kutaongeza hamasa kwa watumishi ili waweze kufanyakazi kwa bidii na kuongeza ubunifu.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango alipokuwa akiweka jiwe la msingi jengo la utawala la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Amewataka wahakikishe wanaongeza mapato na kuweza kujiendesha kibiashara.
Aidha, ameitaka mamlaka hiyo kuendelea kushirikiana na jamii ili kuthibiti tabia ya ujangiri.
Vilevile, ameitaka mamlaka hiyo kuendelea kuboresha mifugo na upatikanaji wa Maji kwa mifugo ya wananchi ili kuendelea kujenga mahusiano mazuri na wananchi.
Nae, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kukamilika kwa jengo hilo kutaongeza ufanisi wa kutuo huduma kwa watendaji .
Pia, mradi huo utapunguza gharama za uwendeshaji kwa mamlaka hiyo kwani wataweza kufanya kazi nje ya hifadhi za Ngorongoro.
Amewataka wananchi waendelee kufuata sheria, Kanuni na taratibu za uhifadhi ili kupunguza uvamizi wa maeneo ya uhifadhi.
Akisoma taarifa ya ujenzi Naibu Muhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro Elibariki Bajuta amesema ujenzi huo umefanyika kwa lengo la kupisha uhifadhi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro uliokuwa umevamiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu.
Amesema ujenzi huo umegawanyika katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ni ujenzi wa jengo la Utawala, nyumba ya muhifadhi pamoja na nyumba za manaibu wahifadhi ambao utagharimu kiasi cha bilioni 10.4 hadi kukamilika kwake.
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuanzia Julai hadi Aprili 2023 walipata jumla ya wageni 612,252 na malengo yao ni kupata wageni 1,200,000 ifikapo 2025/2026.
Mamlaka ya hifidhi ya Ngorongoro ilichukua uwamuzi wa kujenga jengo la utawala nje ya hifadhi ikiwa ni moja ya utaratibu wa kuhifadhi mazingira ya hifadhi hiyo dhidi ya shughuli mbalimbali za kibinadamu zilizokuwa zinaathiri hifadhi hiyo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.