Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Balozi Mary O'neill, amefika mkoani Arusha na kumtembelea Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella ofinisini kwake leo Machi 25, 2024.
Balozi Mary licha ya kusaini kitabu cha Wageni, amefanya mazungumzo Mafupi na Mkuu huyo na kumkabidhi zawadi ya Kalenda ya mwaka 2024.
Hata hivyo Mhe. Mongella amemkaribisha Balozi huyo mkoani Arusha na kumhakikishia hali ya usalama muda wote awapo mkoani Arusha huku akifurahia hali ya hewa nzuri ya Mkoa wa Arusha na vivutio vya utalii vinavyopatikana mkoani humo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.