Viongozi wa Umoja wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wamefika kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. John V. K Mongella jioni ya leo Januari 24, 2024.
Viongozi hao, wakiongoza Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya, licha ya kusaini kitabu cha wageni, wamefanya kikao kifupi na Mkuu wa Mkoa na kujadili maandalizi ya Sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi inayotarajiwa kufanyika Kitaifa Mkoani Arusha, Mei, 2024.
Hata hivyo, Mhe. Mongella licha ya kuwakaribisha viongozi hao mkoani Arusha, amewaahidi kutoa ushirikiano muda wote wa maandalizi ya Sikukuu hiyo, kadri Maelekezo yatavyotolewa na viongozi hao kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na taratibu za Serikali
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.