Na Elinipa Lupembe.
Wananchi wa Tarafa ya Ketumbeine wilaya ya Longido, wametakiwa kuwa watulivu, na kujikita kwenye shughuli za maendeleo, kwa kuwa Serikali yao ya awamu ya sita, imejipanga vema kutatua kero na changamoto zinazowakabili, katika maeneo yao kisekta.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, mara baada ya kupokea kero zinazowakabili wananchi hao, wakati wa mkutano wa Hadhara uliowakutani wakazi wa Tarafa ya Ketumbeine, uliofanyika kijiji cha Lopolosek.
Mhe. Mongella amesema kuwa, lengo la Serikali ya mama Samia ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za msingi kwa kuzifikisha huduma hizo kwenye maeneo yao, huku kipaumbele cheke zaidi ni wananchi waishio maeneo ya vijijini.
Aidha, katika kutatua kero hizo, amemuagiza Mkuu wa wilaya hiyo kupitia ofisi ya Mkurugenzi, kujenga mara moja chumba cha kuhifadhia maiti kaatika kituo cha afya Ketumbeine, kwa kuwa, ukosefu wa Mochuari, unasababisha wananchi kuingia gharama kubwa kufuata huduma hiyo maeneo ya mbali, pindi wanawapoteza wapendwa wao na kumtaka mkurugenzi kujenga choo kwenye soko la Ketumbeine ifikapo Machi 30, 2024 viwe vimekamilika.
Hata hivyo, Msimamizi wa Kitengo cha Matengenezo TANROAD Arusha, Injinia Reuben Jairo, amesema kuwa, fedha za usanifu wa barabara zimetengwa kwenye bajeti, wapo kwenye hatua za awali za kuandaa makabrasha kwa ajili ya kutengenza barabara hiyo kiwango cha lami kwa urefu wa Km 98 kutoka Longido - Oldonyolengai kuelekea Ngorongoro, kama wananchi hao walivyoomba miaka miwili iliyopita.
Naye Meneja wa TARURA Wilaya ya Longido, Injinia Laurence Msemo, amethibitihsa kuongezeka kwa bajeti ya barabara hadi kufikia bilioni 3.5, fedha ambazo zitawezesha matengenezo ya barabara zote za Longido kwa awamu, licha ya uharibifu unaotokana na mvua zinazoendelea kunyesha, huku akithibitisha kuomba bajeti ya ziada ya kufanya ukarabati wa barabara hizo.
Akijibu kero ya maji katika shule ya shikizi ya msingi Kale, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Longido, amesema kuwa, mradi wa bilioni 1.3 unaotekelezwa kwenye kata ya Ketumbeini utahusisha maeneo yote ya kata hiyo na vijiji vyake licha ya kuwa ulichelewa kidogo katika utekelezaji wake.
Kuhusu suala la umeme wa REA kufikia vitongoji vitatu vya Kijiji hicho cha Lopolosek, Meneja wa REA wilaya ya Longido, amesema kuwa, mafundi wapo kazini wanaendelea na kazi ya za kusambaza umeme kwenye vitongoji baada ya kukamilisha usambazaji kwenye vijiji vyote.
Awali wananchi hao, waliwasilisha kero zao , ikiwemo ukosefu wa mochuari kituo chao cha afya, ukosefu wa choo soko la Ketumbeine, kutokufikiwa na
umeme baadhi ya vitongoji, ubovu wa barabara za ndani pamoja na uhaba wa maji unaosababisha mgao kijiji cha Kale
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.